Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma kali kama Siachani nawe na Jichunge ambaye iasili anatokea pande za Mwanza hapa Tzee mkoa ambao msanii mwingine mkali Mo Music ametokea, amesema hashindani na msanii mwenzake huyo zaidi ni marafiki.
Mo music ambaye alichukua headlines vilivyo kutokana na ngoma yake ya 'Basi nenda' ilionekana kama kapotezwa naujio wa Baraka kiasi kwamba hits zake nyingine alizotoa baada ya 'Basi Nenda' kutopata air time ya kutosha na hata kutokujulikana sana na watu.
Akiwa kwenye interview Planet Bongo ya EARadio leo jumamosi, Baraka amekana madai ya kufanya music ili amfunike Mo music na kusema kuwa wao ni zaidi ya marafiki na isitoshe wanatoka mkoa mmoja. Zaidi ya yote ameushukuru uongozi wake kwa kumfikisha alipo.
Kumbuka kuwa Baraka Da' Prince yupo kwenye tuzo za KTMA akiwania tuzo ya msanii bora anayechipukia, fanya kama kumpigia kura hivi kama unahisi anastahili nishani hiyo.
0 comments:
Post a Comment