Leo ni moja kati ya siku zilizokuwa zikisubiriwa sana kwa wapenda burudani hasa Africa masariki kutokana na tukio husika lina wahusisha watu maarufu wawili ukanda wa Afrika Mashariki na inasemekana ni moja kati ya couple zinazopendwa zaidi ukanda huu.
Hapa Zari pale Diamond kwa pamoja wanawajaza watu pande za Mlimani city kush
uhudia tukio la kipekee na la kihistoria kwa Tanzania liitwalo 'Zari All White Party'. Mbali na tukio hilo pia ni siku rasmi kwa wapenzi hao kuzindua rasmi 'TV Reality Show' yao ambayo kwa mujibu wa Diamond ni moja kati ya vipindi bora vya luninga Tanzania.
Akiongea kwenye kipindi cha Power Breakfast pamoja na Clouds360 vyote vya Clouds FM/TV asubuhi ya leo ambapo mahojiano hayo yalikuwa yakirushwa redioni na kwenye TV moja kwa moja Diamond alisema, "Tunaandaa kitu cha tofauti na sio tufanye tu, kitakuwa kipindi bora ambacho kila mtu atafurahi kukiona na kitasubiriwa kwa hamu kama vipindi vingine vikubwa vya TV."
Tusubiri. Ila tunakutakia kila la kheri katika harakati zako.
0 comments:
Post a Comment