Followers

Wednesday, 6 May 2015

JOYCE KIRIA ASHINDA KESI YA MBUNGE NA MTOTO MLEMAVU

Hatimaye ile kesi ambayo ilimuhusisha mwanadada mwanaharakati Tanzania akitetea haki za wanawake na watoto, Joyce Kiria mtoto mlemavu (Abbas) ambaye alikuwa ametelekezwa na baba yake mzazi ambaye ni Mbunge wa Zanzibar (jina limehifadhiwa) imefikia mwisho na Joyce kuibuka mshindi wa kesi hiyo.



Joyce Kiria akiwa amembeba mtoto mlemavu (Abbas)

Kwenye kesi hiyo Mbunge huyo alituhumiwa kwa kumtelekeza mtoto huyo mwenye ulemavu ambapo kulifunguliwa kesi mbili moja ikiwa mahakama ya Kisutu. Lakini baadae Joyce alitumiwa demand note ya kumdai fidia ya millioni 500 kwa madai kuwa amedhalilishwa.
Joyce Kiria kwenye mahojiano na Mama Abbas huku akiwa amembeba mtoto Abbas mwenye ulemavu.

Kupitia akaunti yake ya facebook, Joyce amepost ujumbe huu:
Onja shangwe na Nderemo za kushinda kesi ya Mbunge aliyetelekeza mtoto uuuuuuwiiiii inakujia Eatv na bloguni soon.... I love me my self and I jamani dunia Tumeshiiiiiindaaaaaàaa... Nacheza kwanza nikipumzika ntakupa mkanda mzima😅😅😅😅

Acha tusubiri...

Onja shangwe na Nderemo za kushinda kesi ya Mbunge aliyetelekeza mtoto uuuuuuwiiiii inakujia Eatv na bloguni...
Posted by Joyce Kiria on Thursday, 30 April 2015

0 comments: