Usiku wa tarehe 23.05.2015 kwenye ukumbi wa Mwl. Nyerere Posta, kulitokea tukio jingine kubwa la kiburudani kwenye industry ya movie hapa bongo la kwanza kutokea,
Ilikuwa ni utoaji wa tuzo kwenye filamu zilizopewa jina la (TAFF).
Katika tuzo hizo zilizoandaliwa na Shirikisho la Bongo muvi likiongozwa na Rais wake Simon Mwakifamba waliandaa tuzo hizo kwa mara ya kwanza katika hisoria ya muvi na kumualika Waziri wa Ytamaduni na Michezo Mh. Fenela Mkangala kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hizo huku kulikuwa na wageni kibao kutoka ndani na nje ya nchi kiujumla.
Katika tuzo hizo ambazo wasanii kibao walipata tuzo ikiwemo hadi wale ambao wamefariki lakini mchango wao umeonekana kusaidia kutangaza filamu zetu nje, Baadhi ya watu fanikiwa kupata tuzo hizo ni : Mzee Majuto, Irene Paul, Grace Mapunda, Steven Kanumba, Tinno, John Kallage, Zamaradi Mketema, Mzee Jangala, n.k
Hizi hapa ni baadhi ya picha zikionyesha jinsi tukio hilo lilivyokuwa.... Enjoy!!
0 comments:
Post a Comment