Jeshi
la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi
Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la
kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la
utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya
saa moja jioni.
Bomu hili
linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa
hatua zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo
ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao
za kila siku.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu
wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili
linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka
jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu
waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi
watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.
Msikhela
amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa
wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini
watu wanaousika na matukio ya namana hii.
Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari
watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,
walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono
ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe
mjini songea mkoani Ruvuma.
Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na
mtandao huu wa demasho kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho
cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika
mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha
amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama
watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo
hivi.
0 comments:
Post a Comment