Followers

Tuesday, 28 October 2014

SHUHUDIA PICHA ZA JWTZ WAKITEGUA BOMU KATIKA ENEO LA KITUO CHA KURUSHIA MATANGAZO CHA TBC SONGEA

Bomu lililotengenezwa kienyeji  kama linavoonekana katika picha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.

Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa polisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavyoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini

Bomu lililotengenezwa kienyeji

Mtaalamu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.

Mtaalamu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha  kulitegua bomu bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii.

0 comments: