Followers

Tuesday, 28 October 2014

JE WAJUA KILICHOMFANYA DOMINICA KURUKA UKUTA WA IKULU MAREKANI SOMA HII

 http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/10/White-House-jumper-jpg.jpg

 

Adesanya

Habari zinasema hii si mara ya kwanza kwa Mnigeria Dominica Adesanya (23) kuruka ukuta wa White House, na safari hii baada ya kumfikisha mahakamani imebainika kuwa ana tatizo la akili hivyo hawezi kushitakiwa akiwa na hali hiyo.

Daily Mail imeripoti kuwa baada ya mahakama kuthibitisha vipimo kutoka hospitali kuwa ana tatizo hilo, mahakama iliamuru awekwe chini ya ulinzi huku akipata matibabu ya ugonjwa huo mpaka Desemba 22 kesi yake itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Adesanya ametolewa mahakamani hapo akipiga kelele za kuomba msaada huku akilaumu kitendo cha kukamatwa kwake.

Hii ni mara ya pili kwa Mnigeria huyo kuruka ukuta wa White House, ambapo mara ya kwanza Adesanya ambaye ana asili ya Nigeria kufanya hivyo ilikuwa Julai 27 majira ya saa 4 usiku mwaka huu, na kurudia tena Oktoba 23 majira ya saa 1 jioni.


0 comments: