Msanii wa
sanaa ya maigizo kutoka Tanza comedy(Tanzania comedy Association),Joseph
Salonge (Kamugisha),wiki hii amefunga Ndoa na mchumba wake wa siku nyingi,na
aliye dai kumpenda sana.
Kamgisha
ambaye pia amecheza katika sinema na Tamthiliya tofauti hapa nchini ikiwemo
Milosis na Dirty Game kutoka Tuesday Entertainment. ametoa shukrani za dhati
kwa wote walio fanikisha sherehe yake kufanikiwa.
Akizungumza
na mwandishi wetu Kamugisha alionyesha
kuwa na furaha alipenda pia kuweka wazi ndoa yake kufuatia na baadhi ya watu
kutoamini kuhusiana na ndoa yake.
“Napenda
kuweka wazi kuwa kwa sasa nimeoa na wote wasio amini naomba waamini kuhusu hilo napenda kutoa
shukrani zangu za dhati kwa wasanii wenzangu na wote waliofanikisha sherehe
yangu.”
“kiukweli napenda kusema kuwa nampenda sana mke wangu...” alisema Kamugisha
Wakati huohuo kamugisha alipenda kuzungumzia kuhusu kazi
inayo tengenezwa na Mbalamwez Arts chini ya mkurugenzi Ibrahim Msuka inayo
karibia kuanza hivi karibuni inayo husu Familia za kitanzania ambayo itaanza
kurushwa hivi karibuni na moja kati ya vituo vya Televisheni hapa nchini.
Kamugisha kushoto akiwa amembeba mke wake baada ya kutoka kanisani.
Kamgisha akiwa katika pozi la ufukweni na mke wake.
0 comments:
Post a Comment